Jeshi la Wanamaji nchini Kenya limewakamata wavuvi haramu109 raia wa Tanzania kwa kosa la kushiriki katika uvuvi eneo la bahari ya Hindi upande wa nchi hiyo.

Wavuvi hao wamekamatwa katika eneo la Shimoni linalomilikiwa na bandari kusini mashariki mwa Kenya karibu na mpaka wa Tanzania na kuwasilishwa mbele ya mahakama ya kaunti ya Kwale.

Aidha, Wavuvi hao walikamatwa mara baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi 20,000 za Kenya kila mmoja kwa mujibu wa Gazeti la Biashara nchini Kenya Business Daily.

Serikali ya Tanzania tayari imeanza mchakato wa kuhakikisha kuwa raia hao wanaachiliwa huru ili waweze kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

“Tayari tumezungumza na Wizara ya Mambo ya Nje na jeshi la polisi nchini Kenya ili kuweza kutatua tatizo hilo lililojitokeza kwa wavuvi hao,”amesema Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega.

Hata hivyo, Tanzania na Kenya zimekuwa katika mgogoro wa kibiashara ambao umekuwa ukizua uhasama katika ya mataifa hayo jirani.

 

Video: Barua ya Serikali kwa KKKT sarakasi tupu, NACTE yafuta usajili vyuo 20
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Ubelgiji