Chama cha wavuvi wadogo wadogo Minazi Mikinda (CHAWAWANI), kata ya kivukoni kimeomba wizara husika kuingilia kati changamoto za kanuni za uvuvi kwakuwa zilizopo si rafiki kwao.

Chama hicho kimesema changamoto za kanuni ikiwamo faini kubwa zinazotozwa zimesababisha wavuvi kutoingia baharini kwa zaidi ya siku tano sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kaimu Mwenyekiti wa Chawawani, Idd Darusi amesema mabadiliko ya kanuni za uvuvi yamesababisha kusitisha ajira za wavuvi zaidi ya 1o, ooo katika eneo hilo sambamba na maeneo mengine yanayojishughulisha na sekta hiyo nchini.

” Mabadiliko yaliyoanzishwa na kanuni za mwaka huu si rafiki kwetu kwa mfano mtego wa dagaa inabidi utumike wakati wa usiku tu, jambo hili kwetu sisi wavuvi linatuweka katika mazingira magumu ya utendaji kazi” amesema Darusi

Ameongeza kuwantangu mwaka 2008 hadi sasa kumekuwa na mabadiliko kadhaa katika sekta ya uvuvi, ambapo mwaka 1995 kuliondolewa uvuvi wa kutumia kokolo na kuwepo uvuvi wa kutumia nyavu ya mtando ambayo pia inaendelea kutafsiriwa vibaya na baadhi ya maofisa uvuvi na watafiti.

Amesema wanashangaa kusikia kutoka kwa maofisa uvuvi kuwa nyavu ya mtando inafaa kutumika mchana na si usiku na yeyote atakaye kwenda kinyume atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini.

Mratibu wa Fungamano la Uvuvi wa sekta ya Uvuvi Ukanda wa Pwani, Mohamed Said, ameiomba Serikali kumaliza kero za wavuvi ambazo ni zamuda mrefu kwakuwa sekta hiyo inachangia pato la taifa kwa asilimia kubwa.

Hatma ya Alliance FC, Ndanda FC kujulikana leo
PICHA: Liverpool wakabidhiwa kombe la Ubingwa EPL