Wawekezaji kutoka nchini Misri wamewasili kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Serikali ili waweze kupata nafasi ya kuwekeza katika Sekta ya Viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu na kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli ambaye anataka kuibadili Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Aidha, Ujumbe huo wa wawakezaji kutoka Misri umekuatana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  pamoja na wawakilishi toka Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa (TIC) kwenye Ofisi ndogo ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Wawekezaji hao wamesema kuwa wanadhamira kubwa ya kuwekeza kikamilifu hapa nchini ili kuiwezaTanzania kuzalisha Dawa za bindamu hapa hapa nchini.

“Lengo letu sisi ni kujenga kiwanda kikubwa ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha dawa ambazo zitawahudumia watanzania pamoja na nchi za Afrika Mashariki na ya kati,”amesema mmoja Wajumbe hao.

Kwa upande wake Waziri, Ummy amewaahidi wawekezaji hao kuwasaidia katika mipango ya ujenzi huo na kutoa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha viwanda hivyo vinajenga nchini kwa muda uliopangwa.

“Naelekeza kwa taasisi zote zitakazoguswa na uanzishwaji wa viwanda hivi watoe ushirikiano wa hali ya juu ili lengo hili lifikiwe, soko la dawa hapa nchini lipo naomba niwahakikishie hili”amesema Ummy.

Hata hivyo, Ummy amewaomba wawekezaji hao kuharakisha ujenzi wa viwanda hivyo ndani ya miezi kumi na nane kama walivyo ahidi ili watanzania waanze kunufaika mapema na huduma za viwanda hivyo.

Video: Majina watakao wania tuzo EJAT yatangazwa
Makamba atoa neno kuelekea Maadhimisho ya Muungano