Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa wawekezaji wanaokusudia kuanzisha biashara zao Zanzibar washirikiane na jamii kusaidia masuala mbalimbali kama vile elimu, maji na afya.

Alhaji Dkt. Mwinyi meyasema hayo hii leo Mei 26, 2023 baada ya swala ya Ijumaa katika ufunguzi wa msikiti wa Masjid El-Marhoum Abdel Moeim Shahein uliopo Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema wawekezaji wanapaswa kuona umuhimu wa kusaidia jamii inayowazunguka pale wanapowekeza, na kuhakikisha kwamba wanachangia kwa hali na mali ili kuboresha uhusiano wao na jamii hiyo.

Katika hotuba yake Rais Dkt. mwinyi pia alibainisha kuwa nia na madhumuni ya msikiti huo ni kutoa fursa ya kufanya ibada na kuwafundisha vijana katika madrasa iliyopo msikitini hapo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 27, 2023
Vifo vya mfungo Kenya: Majambazi wenye silaha walisimamia zoezi