Jeshi la Polisi nchini Ubelgiji linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kupanga njama ya kufanya Shambulizi la Kigaidi jijini Brussels katika mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Ubelgiji la RBTF,  watu hao walikamatwa Brussels  katika eneo la Flemish Brabant.

Polisi waliwakuta watu hao wakiwa na mavazi ya kijeshi pamoja na vifaa vya kompyuta. Lakini hawakuwakuta na aina yoyote ya vilipuzi wala silaha.

Ubelgiji imekuwa katika tahadhari kubwa tangu yalipotokea mashambulizi ya kigaidi jijini Paris Ufaransa, Novemba 13 mwaka huu yaliyotekelezwa na kundi la IS.

Taarifa za kiupelelezi zilieleza kuwa watu waliopanga na kutekeleza mashambulizi hayo jijini Paris walitokea nchini Ubelgiji.

CUF Yapinga Kilichosemwa na CCM kuhusu Mazungumzo ya Mgogoro wa Uchaguzi
Ni Leicester City Vs Manchester City