Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa ajali iliyohusisha magari matatu iliyotokea hii leo Novemba 9, 2022 katika eneo lenye mteremko wa Iwambi na kusababisha vifo vya watoto wawili wa familia moja.

Kamanda Kuzaga amesema, chanzo cha ajali hiyo iliyotokea hii leo Novemba 9, 2022 ni mwendo kasi wa gari aina ya fuso lenye namba za usajili T.601 DXC, huku mashuhuda wakisema tukio hilo limetokea majira ya saa 12:45 asubuhi na chanzo cha ajali kikidaiwa kuwa ni mwendo kasi.

Moja ya ajali zilizohusisha Basi dogo la Abiria.

Imeshuhudiwa kuwa, Dereva wa basi hilo dogo la Abiria katika jitihada za kulimudu gari lake alishindwa baada ya kugongana ubavuni na gari hilo dogo aina ya Totota Raum lenye namba za usajili T.452 DHD.

Kamanda amesema, “Gari hilo T.601 DXC Fuso Bus liliendelea kugonga gari jingine lenye namba za usajili T.673 DMV lenye Tela namba T.362 DMG aina ya Scania lililokuwa linaelekea Mbeya na gari namba DAD 3981 na Tela lake ABF 75591 aina ya Dofeng”

Kufuatia ajali hiyo, Kamanda Kazuga amewaomba madereva kuwa waangalifu wakati wakiendesha vyombo vya moto, ili kuepusha ajali na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

TEF yapendekeza Wavuvi kuandaliwa Jeshi la akiba Uokozi
Gazeti la L'Equipe lachafua hali ya hewa