Gwiji wa soka nchini England Alan Shearer, amempa ushauri wa bure nahodha na mshambuliaji wa Man Utd Wayne Rooney ambaye kwa sasa anapita katika kipindi kigumu.

Shearer, ambaye alistaafu soka akiwa na klabu ya Newcastle Utd mwaka 2006 ameonyesha kuguswa na changamoto anazozipitia mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kutamba akiwa na Everton kabla ya kuhamia Man Utd.

Shearer amemtaka Rooney kuwa mstahamilivu na mvumilivu huku akikubaliana na hali halisi iliyo mbele yake kwa sasa, ya kurejea katika kiwango chake huku akimtaka kuiga mfano wa Steven Gerrard na Frank Lampard.

Amesema wawili hao walifikwa na majaribu wakiwa katika vikosi vya Liverpool na Chelsea lakini walijikubali na kukabiliana nayo na hatimae walifanikiwa kuondoka kwa heshima na kutimkia nchini Marekani.

Gerrard ambaye bado anatambulika kama shujaa wa muda wote wa Liverpool aliamua kuelekea Marekani na kujiunga na LA Galaxy mwaka 2015, ili hali Lampard aliondoka Chelsea na kuelekea New York City, ambao walimtoa kwa mkopo Man City, lakini maamuzi hayo yalifanyika baada ya kuthibitisha uwezo wao na mashabiki kukubali walichokifanya.

Image result for alan shearer and wayne rooneyAlan Shearer (Kushoto) akisaka mbinu ya kumuhadaa Wayne Rooney (Kulia) katika moja ya michezo ya ligi kuu ya soka nchini England

“Kuna watu wawili ambao Wayne Rooney anapaswa kuwafuata kama kigezo chake, hasa katika kipindi hiki kigumu, naamini akifanya hivyo atafanikiwa,” Ameandika Shearer katika taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la The Sun.

“Steven Gerrard na Frank Lampard waliwahi kufikwa na mkasa kama wa Rooney, lakini walisimama na kutambua nini walichotakiwa kukifanya.

“Inafahamika kwa sasa Rooney hana nafasi katika kikosi cha Man Utd na hata upande wa timu ya taifa, ninamshauri atafute mahala pengine pa kucheza soka ambalo litampa changamoto mpya.

“Ilimchukua Gerrard miaka 17 akiwa na Liverpool na Lampard miaka 13 akiwa Chelsea, na walipita katika hali kama ya Rooney ya sasa hivi.

Rooney amekua akishauriwa na watu wengi kuhusu mpango wa kuachana na Man Utd na kufikiria kujiunga na klabu nyingine za England ama nje ya nchi hiyo, huku wengine wakimtaka afikirie kwenda China ama Marekani kucheza soka, jambo ambalo Shearer ameliunga mkono.

Lowassa aumulika mwaka mmoja wa Magufuli, 'maisha yamezidi kuwa magumu'
Siri Za Yanga Na George Lwandamina Zaendelea Kufichuka