Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya England, Wayne Rooney amethibitisha kustaafu soka la kimataifa mara baada ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ambazo zitafanyika nchini Urusi.

Rooney, mwenye umri wa miaka 30, amekua katika timu ya taifa ya England tangu mwezi Agosti mwaka 2003, na kwa sasa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika timu hiyo kwa kufunga mabao 53 katika michezo 115 aliyocheza.

Rooney amethibitisha kustaafu soka utakapofika wakati huo, alipozungumza na waandishi wa habari, kuhusu maandalizi ya kikosi cha England kuelekea katika mchezo wa kuwanai kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ambapo watapambana na Slovenia.

Chelsea Waushtua Ulimwengu Wa Soka
AS Roma Waonyesha Nia Kwa Jack Wilshere, Lakini Waomba Msaada