Wazee jijini Arusha wamemuomba Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli  kuwasaidia kupata mafao yao ya iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa baraza la wazee, Mathius Kichao alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa hadi sasa kuna baadhi ya wazee ambao hawajalipwa stahiki zao.

“Kuna muda wazee hawa waliandamana jijini Dar es salaam, wengine wakalala barabarani lakini viongozi wa wakati huo hawakuona thamani ya kilio kile, wakawafukuza bila kujua machungu waliyokuwa nayo mioyoni kwa kazi kubwa waliyoifanya,”amesema Kichao.

Hata hivyo, wazee hao wameomba viongozi mbalimbali wa dini na Serikalini ili wanapotembelea Arusha wawawone ili waweze kuwapatiwa ushauri wa namna ya kuongoza nchi kwa makini zaidi.

Kaburu: Hang'oki Mtu Msimbazi
Hakim Ziyech Adhihirisha Jeuri Yake Kwa Herve Renard