Baadhi ya Wazee ambao ni Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika Wilaya ya Urambo unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameomba malipo wanayopatiwa yaendelee kutolewa kupitia utaratibu wa zamani  wa kuwapelekea fedha badala ya kutumia njia ya mtandoo.

Wametoa kauli hiyo katika Vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Urambo ambao mara baada ya  kukutana timu ya Mkoa iliyokwenda kuangalia matatizo wanayokumbana nayo katika utaratibu mpya wa ulipaji kwa njia ya mtandao.

Wamesema kuwa wengi wao hawana simu na hawajui kutuma simu na hivyo kuwafanya wakati mwingine watafute vijana wa kuwasaidia ambapo baadhi yao huwaibia fedha zao wakati wa kutoa katika mitandao.

Aliongeza kuwa wengine kwa sababu ya kutojua kusoma na kuandika wakati mwingine wakuwa wakishindwa kutunza kumbukumbu ya namba zao siri na hivyo kuwafanya washindwe kupata fedha pindi inapoingia katika line zao.

“Kwa sababu mimi nakuwa sina simu zaidi ya kumiliki line tu, wakati mwingine kwa sababu wengi tunawatumia vijana wetu au majirani wenzetu wamekuwa wakituletea fedha pungufu sababu wengine hatujui kusoma na wala hatuwezi kubisha,”amesema Mzee Rashid.

Hata hivyo, akitoa elimu kwa walengwa katika Vijiji vya Kitete na Sipungu juu ya umuhimu wa matumizi ya mtandao katika upokeaji wa malipo yao, Mchumi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fredrick Aron amesema kuwa hivi sasa malipo yote ya Serikali yatolewa kwa njia ya mtandao kwa hiyo ni vyema wakaendelea kujifunza jinsi ya matumia ya huduma za utoaji wa fedha kwa njia hiyo.

 

Joh Makini aeleza kwanini video za hip hop ‘hazikiki sana’ YouTube
Video: Usiyoyajua sakata la shamba la Sumaye, Uchunguzi 'Makinikia' almasi pasua kichwa