Umoja wa wazee nchini Kenya umeitaka Serikali kuondoa kwenye vitambulisho vya taifa sehemu zinazoonesha mahali ambapo mhusika amezaliwa kwani inahuisha ukabila.

Kenya ni taifa linalokabiliwa na hali ya ukabila hususan kwenye nyanja za siasa na kazi, hali inayosababisha anayechaguliwa kuongoza au kupewa kazi wakati mwingine kuathiriwa na mahali alipozaliwa.

Muasisi wa umoja huo, Martin Kinyanjui amesema kuwa wazee wameamua kuungana kuhakikisha wanajenga umoja wa kitaifa bila kutumia siasa.

“Umoja huu ulitakiwa kuanzishwa mwaka 2016 lakini kwa sababu hatukutaka kamwe kujihusisha na masuala ya siasa, tulilazimika kusubiri hadi michakato ya uchaguzi ikamilike,” alisema Kinyanjui.

Tungependa kuona vitambulisho vya Wakenya vinabadilishwa na kuondolewa kipengele cha eneo anakozaliwa kwakuwa kinachochea ukabila,” aliongeza.

Akihitimisha hotuba yake, Kinyanjui alieleza kuwa umoja huo sio kwa sababu ya watu wenye umri zaidi ya miaka 54 pekee, aliwataka hata vijana kujiunga na umoja huo kwa ajili ya kutoa ushauri.

Video: Mwigulu, 'Niliomba ubunge na si uwaziri', Dege la JPM kutua leo
Chadema wamtumbua Mwenyekiti Siha