Leo Mei 26, 2018 Naibu Waziri wa Afya, Augustine Ndugulile amefanya ziara ya kushtukiza na kutembelea uwanja wa ndege wa Taifa wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere (JNIA) ili kukagua vifaa maalumu vilivyopo kwa ajili ya kupima afya za abiria wanaoingia nchini kubaini kama wanamaambukizi ya ugonjwa wa Ebola.

Amesema kuwa amejiridhisha na  namna ambavyo Uwanja wa ndege wa Taifa wamejiandaa kukabiliana na ugonjwa huo.

”Nimefanya ziara hapa nimejiridhisha na maandalizi ambayo tunayo na kwamba tupo salama na endapo kama kutatokea mgonjwa basi Tanzania tumejipanga vizuri kabisa” amesema Ndugulile.

Ndugulile amesema tayari wameshaanza kusambaza vifaa mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, ameongezea kuwa tayari wameshafanya mazoezi endapo watakutana na mtu mwenye ugonjwa huo kujua hatua gani zitachukuliwa.

Aidha amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha kwamba watu wanajua namna ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola na kuthibitisha kuwa mipaka ya nchi ipo salama na mpaka sasa hakuna mtu yeyote nchini aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa huo.

Mhadhiri auawa kwa kuchomwa kisu
Vikongwe wapewa mafunzo ya kujihami dhidi ya wabakaji