Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Afrika Kusini, Malusi Gigaba amejiuzulu nafasi yake hiyo wiki mbili baada ya kipande cha video inayomuonyesha akijichua kusambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini humo.

Taarifa kutoka ofisi ya rais imesema kuwa Gigaba ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama tawala African National Congress-ANC, kajivua nafasi hiyo kwa heshima ya nchi yake na harakati zinazomhusu.

Waziri huyo amevishutumu vyombo vya usalama nchini Afrika Kusini kwa kudukua simu yake na kuachia kipande cha video chenye urefu wa sekunde kumi na tatu , ambayo alijitetea kuwa alimrekodia mkewe.

Aidha, Gigaba mwenye umri wa miaka 47, miaka ya hivi karibuni amejikuta katika wakati mgumu kutokana na kutumia madaraka yake vibaya katika huduma mbalimbali na kuisaidia familia ya wafanyabiashara ya Gupta yenye utata.

Wafanyabiashara hao wenye asili ya nchini India wanahusishwa sana na kashfa kadhaa za rushwa chini ya utawala wa Rais Jacob Zuma.katika kila hali ikiwa ni pamoja na Bwana Gigaba, wamekana makosa yote wanayotuhumiwa.

Hata hivyo, vyama vya upinzani nchini humo vimekuwa vikimshinikiza raisi Cyril Ramaphosa kumtimua kazi waziri huyo, na kwamba wamepokea kwa mikono miwili kujiuzulu kwake.

Video: Siri ya Rostam kuteta na JPM, Fagio la Magufuli lamtisha waziri
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 14, 2018