Waziri wa Wanawake nchini Nigeria, Aisha Alhassan amejiuzulu nafasi yake na kukihama chama tawala cha All People’s Congress.

Bi. Alhassan aliandika jana barua ya kujiuzulu na kueleza kuwa pamoja na mambo mengine, amesukumwa na tukio la chama hicho kumkatalia kugombea Ugavana katika jimbo la Taraba.

Anakuwa mjumbe wa pili wa baraza la mawaziri katika Serikali inayoongozwa na Rais Muhammadu Bushiri kujiuzulu ndani ya kipindi kifupi.

Wiki mbili zilizopita, Kemi Adeosun aliyekuwa mwangalizi wa masuala ya fedha alijiuzulu na kukihama chama hicho.

Hii ni mara ya kwanza kwa mawaziri kujiuzulu katika Serikali inayoongozwa na Buhari tangu alipoingia madarakani mwaka 2015.

Matukio ya hamahama hasa kwa wabunge nchini humo yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara, wengi wakikihama chama tawala. Mwaka 2019, nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi mkuu.

Video: Mjumbe wa CCM afunguka kuhusu kambi za shule mkoa wa Simiyu
Video: Mhagama azindua ushirika wa makampuni ya matangazo ya biashara

Comments

comments