Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ametengua nafasi ya Meneje wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoa wa Lindi, Mhandisi Isack Mwanawima kutokana na udhaifu wa usimamizi wa barabara za mkoa wa lindi.

Waziri Kamwelwe ametoa taarifa hiyo Julai 31, 2020 kwa vyombo vya habari kuhusiana na kumsimamisha kazi Meneja huyo.

“Kwa kuwa nilishawahi kutoa maelekezo kwa mameneja wa mkoa wa Tanroads kuhakikisha barabara wanazosimamia zinakuwa kwenye hali nzuri na zinapitika,” taarifa hiyo imeeleza.

Pamoja na hayo Waziri amemuagiza mtendaji mkuu TANROADS kupeleka mhandisi mwingine haraka kwaajili ya kuimarisha usimamizi na kufanya matengenezo ya barabara kipande cha Nangurukuru-Mbwemkuru km 90.

Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 30 julai Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitokea kijini lupaso kwenye mazishi ya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Wiliam Mkapa ambapo alipita kwenye barabara ya Nangurukuru-Mbwemkuru na kubaini ubovu wa barabara hiyo km 90.

TMDA: yafungua mashauri 146 makosa ukiukwaji wa Sheria
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 1, 2020