Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Pakistani, Ahsan Iqbal amejeruhiwa kwa risasi na mtu asiyejulikana katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye jimbo la Punjab.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Pakitani, Iqbal mwenye umri wa miaka 59 alipigwa risasi begani leo  akiwa mbele ya umati wa watu waliokuwa wakimsikiliza.

Imeleza kuwa alishambuliwa kwa risasi kadhaa lakini moja pekee ndiyo iliyompata na kumjeruhi kisha alikimbizwa hospitalini.

“Risasi moja ilimpata kwenye bega la kushoto. Amehamishiwa kwenye hospitali ya wilaya ambako anaendele kupatiwa matibabu,” Jam Sajjad Hussain, msemaji wa kitengo cha uokoaji cha nchi hiyo aliiambia Aljazeera.

Serikali ya jimbo hilo pamoja na familia yake kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa waziri huyo hayuko katika hali inayohatarisha maisha yake kwani alipata jeraha dogo.

Ofisi ya Waziri Mkuu, hahid Khaqan Abbasi imetoa tamko la kulaani vikali tukio hilo na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuanza uchunguzi haraka.

Pakistani iko katika wakati wa kampeni ikitarajia kufanya uchaguzi wa wabunge mwezi Julai mwaka huu.

JPM aagiza Machinga waruhusiwe Stendi mpya Msamvu
Simba kujinyakulia kombe kilaini msimu huu, waibuka na ushindi 1 bila