Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia , wazee na watoto, Ummy Mwalimu amesema mtu yeyote atakayepata virusi vya Corona nchini Tanzania atatibiwa katika maeneo yaliyotengwa yaliyopo mkoani Kilimanjaro, Dar es salaam na Mwanza.

Akizungumza mjini Dodoma leo Januari 29, 2020, amesema wizara inaendelea kujiandaa kukabiliana na tishio la ugonjwa huo endapo utaingia nchini.

” Maeneo hayo ni Mawenzi (Kilimanjaro), Buswelu (Mwanza) na Kigamboni (Dar es salaam), wizara itaendelea kujiandaa kukabaliana na tishio la ungonjwa huu endapo utaingia nchini, Tutahakikisha tunapata vifaa kinga, dawa na vifaa tiba vya kutosha” amesema Waziri Mwalimu.

Amesema wanafanya uchunguzi kwa wasafiri wote kutoka bara la Asia, kwenye mipaka na wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege vilivyopo Dar es salaam, Kilimanjaro na Mwanza.

Pia amesema wanafanya uchunguzi katika bandari ya Dar es salaam, wiki mbili zilizopita walichunguza watu 1520 walioingia nchini kutokea China kupitia bandari hiyo na waliotumia mipaka mbalimbali na viwanja vya ndege.

Amebainisha kuwa Wizara inavyo vipima joto 140 ( vya mkono 125 na vya kupima watu wengi kwa mpigo 15) ambavyo vimefungwa kwenye mipaka.

Fahamu zaidi kuhusu virusi vya Corona
Video: Historia fupi ya marehemu Doglas, mwandishi TBC, ''Mwili uligundulika siku ya nne, ulianza kutoa harufu''