Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amevunja Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), baada ya kubaini kuwa Tume hiyo ilipitisha majina ya wanafunzi 486 wasio na sifa kusomea Shahada ya Elimu.

Profesa Ndalichako ametangaza uamuzi huo leo ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi baadhi ya Maafisa wa Tume hiyo waliobainika kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Kutokana na uamuzi huo, Profesa Ndalichako amewateua maafisa wengine watakaokaimu nafasi hizo zilizoachwa wazi.

Februari mwaka huu, Profesa Ndalichako alipitisha fagio katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB) na kumtimua aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo,  George Nyatenga.

 

Rais Magufuli amteua Mizengo Pinda kushika nafasi hii
Rais Akataa kuishi Ikulu akidai kuna ‘Mizimu na Mashetani’

Comments

comments