Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma, na Utawala Bora, Angela Kairuki,ameagiza kusimamishwa kazi kwa maofisa washauri 106 wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Maofisa hao ni wale walioshindwa kufuatilia na kusimamia mpango wa kunusuru kaya masikini na kuingiza watu 55,692 wasiostahili kwnye Mpango huo katika halmashauri zao.

Aidha,ameagiza kusimamishwa kazi kwa maofisa watano waandamizi wa mfuko huo walioko kwenye ofisi za makao makuu, wenye majukumu ya kusimamia mpango huo na mameneja uratibu na mkurugenzi wa uratibu.

Ametoa maagizo hayo kwa Mkurugenzi wa TASAF, Ladslaus Mwamanga  kutokana na watumishi hao kushindwa kusimsmia majukumu yao ipasavyo.

“Nilisisitiza  uhakiki wa kutambua kaya masikini ufanyike kwa uwazi, na kuelekeza malipo yasitolewe iwapo halmashauri  haitafanya uhakiki kwa wakati”amesema Kairuki.

Hata hivyo, Kairuki amesema kuwa baada ya kukamilika kwa uhakiki, jumla ya kaya 55,692 zilibzinika kuwepo kwenye mpango huo bila kustahili, ambapo amesema sababu zilizopelekea kupatikana kwa idadi hiyo kuwa ni pamoja na walengwa kufariki, kaya kuhamia kijiji/mtaa  mwingine ambapo mpango huo haujaanza kutekelezwa na walengwa kujitokeza zaidi ya mara moja.

TPA yapokea msaada wa Bilioni132/- za upanuzi wa bandari
Chuo cha sanaa Bagamoyo hatarini kumezwa na Bahari