Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa bei elekezi ya maji iwe Shilingi 1,300 kwa uniti badala ya 3,000 kwa unit Wilayani Karatu, na kuelekeza kuwepo kwa chombo kimoja kitakachosimamia utoaji wa huduma ya maji katika mji huo

Waziri Aweso, ameagiza pia kuungana kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA), na Mamlaka ya Utoaji wa Huduma ya Maji Vijijini (KAVIWASU), kutengeneza chombo kimoja ambacho kitatoa huduma kwa wananchi.

Waziri Aweso amesema, Serikali itatoa shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji wa Wilaya hiyo na kuagiza mamlaka husika, zianze kutangaza zabuni ya mkandarasi atakayetekeleza mradi wa kusambaza maji.

Amesema, uwepo huo wa chombo kimoja utawezesha maslahi ya wananchi ikiwemo utoaji wa huduma bora za maji pamoja na kuhakikisha miundombinu ya maji haiharibiki.

Aidha, amesisitiza kuwa hakuna mtumishi yoyote atakayefukuzwa baada ya kuungana kwa KARUWASA na KAVIWASA kwani lita zaidi ya milioni 6 zitakuwepo ndani ya mamlaka moja ambazo zitakidhi mahitaji ya wakazi wa wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine, Aweso pia ameagiza bei mpya itatozwa wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji( EWURA) ikiendelea kuchakata bei halisi itakayotozwa kwa wananchi.

Majaliwa ataka usimamiaji falsafa huduma kwa Watanzania
Shambulio ndege zisizo na rubani laua kiongozi wa Al Qaeda