Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amefanya kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ambapo ametoa maagizo ili kukabiliana na upungufu wa maji.

Aweso amewataka wa Mamlaka hiyo kufanya kazi usiku na mchana na kuhakikisha migao ya maji inatolewa kwa uwiano na bila upendeleo.

Amesema hayo wakati akifanya kikao na watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Novemba 17, 2021.

Pia, ameitaka DAWASA kutoa bei elekezi kwa watoa huduma binafsi wa maji kupitia magari( bowsers).

Aidha Waziri Aweso ameahidi ushirikiano wa Wizara katika kukabiliana na changamoto zilizopo.

Mradi wa jifunze uelewe wazinduliwa
Serikali yazindua mkakati wa kitaifa wa magonjwa yasiyoambukiza.