Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kuwa hatashindwa kuendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwapokonya kazi wakandarasi wanaosuasua ikiwemo wanaokwamaisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini.

Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha watumishi wa sekta ya maji mkoani Tanga ambapo amesema katika kutekeleza tayari ameshawafuta kazi jumla ya wakandarasi 118 pamoja na makampuni 69.

“Uhandisi wa maji ni pamoja na kufuatilia miradi uliyopewa na kujiridhisha kama huduma ipo, pale unapo sema Mradi umekamilika basi inamana unatoa maji kwa asilimia 100% na sio ujanja ujanja” Waziri Aweso.

“Sasa unajenga chanzo, unajenga tenki la maji, unatandaza vituo vya maji halafu unaagiza pump miezi sita watu wanaona vituo vya maji lakini maji hayatoki unatengeneza malalamiko, manung’uniko na masononeko yalisiyo na ulazima “ Waziri Aweso.

UEFA yamaliza utata ufungaji bora Euro 2020
Vurugu yaibuka timu ya taifa ya Ufaransa