Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa ameigiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuandaa mpango mkakati wa makusanyo ya mirabaha pamoja na takwimu za maeneo yanayotakiwa kulipa mirabaha na kuziwasilisha wizarani mwisho mwa mwezi Septemba.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo leo Septemba 10, 2021 Jijini Dodoma katika kikao chake na Kikosi kazi cha kukusanya maoni ya wadau katika Kanuni ya Leseni na Maonesho kwa Umma ya 2021 kutoka COSOTA kikiwasilisha taarifa ya maoni ya wadau kwa kanuni hiyo.

“Katika kikao ambacho tutakutana baada ya wiki mbili hizi mje na mkakati huo lazima tujue tunakusanya kwa akina nani na wako wapi pamoja na idadi yao, pia ongezeni kasi ya ukusanyaji wa mirabaha Disemba tunatakiwa kutoa gawio kubwa,”alisema Mhe.  Bashungwa.

Amesisitiza kuwa anahitaji kupata makadirio ya makusanyo ya mirabaha hiyo kwa mwaka huu wa fedha  na  kuanzisha utaratibu ambao atakuwa akifuatilia hali ya makusanyo hayo kwa kila mwezi kwa kuhakikisha anapata taarifa.

Pamoja na hayo naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul aliitaka COSOTA kuhakikisha inajipanga zaidi na kujenga utaratibu wa kushirikiana na mashirikisho na vyama vinavyosimamia maeneo ya kukusanya mirabaha ili kutengeneza mazingira rafiki ya zoezi hili la ukusanyaji.

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi alifafanua kuhusu suala la kukamilika kwa mfumo utakao kuwa ukihesabu na kutambua nyimbo zinazochezwa katika vituo vya Redio kuwa unatarajia kukamilika mwezi Oktoba na ndiyo utaanza kufanya kazi rasmi.

” COSOTA mna kazi kubwa ya kufanya na kuhakikisha mnakusanya fedha za kutosha ili gawio la mwezi Disemba liwe lenye hamasa kwa Wasanii wetu ni imani yangu kuwa kwa Kanuni hii mpya na viwango hivi mlivyopanga kuwa vinalipika kikubwa katika hili ni kuweka mifumo ya kiteknolojia ambayo itarahisisha makusanyo hayo,”alisema Dkt.Ab

Serikali kukuza sekta ya Uvuvi kupitia zana bora
Moto wateketeza gereza, wafungwa wapoteza maisha