Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Innocent Bashungwa amewaagiza Maafisa wa Elimu wa Mikoa na Wilaya, nchini kuwasimamia Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu wa Masomo, kuzingatia kalenda ya utekelezaji wa mtaala, ili kuwa na ufundishaji na ujifunzaji wenye tija na mahiri.

Amesema hayo wakati wa uzinduzi ya kalenda za utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wathibiti Wakuu wa Ubora wa Shule Kanda leo Jijini Dodoma leo.

Waziri Bashungwa amewaagiza Maafisa Elimu Mikoa, kutoa mafunzo ya matumizi ya Kalenda ya Utekelezaji, katika Halmashauri zenu zote, kabla au ifikapo tarehe 1 Februari, 2022.

Waziri Bashungwa ameitaka Mikoa na Halmashauri, kuwatambua wadau wote wa elimu, waliopo katika maeneo yao na kubaini miradi wanayoitekeleza, kwa kuitembelea na kufanya tathmini ili kuona kama miradi hiyo ina tija katika elimu na kuwaagiza kuhakikisha taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo, iwasilishwe kwa Katibu Mkuu au Tamisemi, kila baada ya miezi mitatu.

Aidha amewaagiza viongozi wa Mikoa , Halmashauri na wakuu wa shule kuhakikisha kutokuwepo na mwanafunzi yeyote wa awali, darasa la kwanza au kidato cha kwanza anatozwa michango kama sharti la mwanafunzi kuandikishwa na kila shule kuhakikisha inakuwa na mwalimu mmoja kwa ajili ya kuandikisha wanafunzi.

Rc Hapi: Serikali haijarejesha ada
Mwijaku akitaka Kiti cha Ndugai