Katika kuendeleza Sera inayolenga kuondoa ubaguzi katika sehemu za kazi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Ajira na Walemavu, Stella Ikupa, ameagiza waajiri nchini kuajiri watu wenye Ulemavu na ambao wana sifa na vigezo stahiki kazini.

Akizungumza katika Warsha ya masuala ya Ajira kwa watu wenye ulemavu Naibu Waziri Ikupa, amesema kuwa kuajiri watu wenye ulemavu ni sehemu ya kuwapa heshima,”Walemavu wengi wamekuwa watendaji kazi wazuri ikilinganishwa na watu wasiokuwa na ulemavu, hivyo ni jukumu la waajiri kuweka mazingira wezeshi kwa Walemavu.

Ameongeza kuwa miongoni mwa sababu zinazowafanya walemavu kushindwa kufanya kazi katika maeneo mengi ni utekelezaji duni wa sheria kuhusu haki za walemavu, mitazamo hasi ya waajiri na kuwepo na mazingira yasiyo rafiki katika sehemu zakufanyia kazi, na ameahidi kuwa Serikari inapanga mikakati ya kuzitaka kampuni zote kuweka mazingira wezeshi kwa Walemavu kufanya kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu Tanznia, Ummy Nderiananga, ameiomba Serikali isimamie sharia ya tozo ya sh. milioni moja, kwa taasisi na kampuni yoyote isiyo ajiri walemavu.

Katika warsha hiyo Walemavu na wadau wa taasisi mbalimbali zinazolea na kutetea haki za walemavu kama CCBRT, CEFA, na ATE walieleza changamoto zinazowakabili na nikwa namna gani Serikali inaweza kuwasaidia katika kuzitatua.

 

Klabu bingwa Amerika kusini yapelekwa Qatar
Ukraine yaiomba Nato kuingilia kati mgogoro wake na Urusi

Comments

comments