Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo ameutaka Uongozi mpya wa Shirika la elimu Kibaha mkoani Pwani kuongeza ubunifu kwa kufanya miradi itakayokuwa na manufaa kwa shirika na Taifa kwa ujumla.

Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati alipokua akiwakabidhi vitendea kazi uongozi huo mpya chini ya mwenyekiti wake, Prof Rafael Chibunda ambaye pia ni makamu Mkuu wa Chuo Cha Kilimo (SUA).

Waziri Jafo Amesema shirika hilo lazima liwe na athari chanya kwa wakazi wanaozunguka wilaya ya Kibaha na hiyo ndio kazi kubwa ambayo Bodi mpya inapaswa kufanya.

” Niwapongeze kwa kuteuliwa kuongoza shirika hili kongwe, mnapaswa kujua mmebeba maono ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere na Rais Dk John Magufuli, nendeni mkafanye kazi kwa kutumia elimu zenu, uwezo wenu na uzoefu wenu. Kayaguseni maisha ya watanzania” Amesema Jafo

Shirika la Elimu Kibaha ni mojawapo ya Shirika kongwe nchini linalotoa huduma ya elimu na afya huku likisaidia mapambano dhidi ya maadui watatu ambao ni Maradhi, Ujinga na Umaskini.

Shirika hilo ambalo limetimiza miaka 50 toka kuanzishwa kwake ni chombo ambacho kimekua kikitoa elimu shuleni na inayohusu afya na kilimo na kutoa tiba na kinga kwa wananchi wanaozunguka maeneo jirani.

Prof Rafael Chibunda amemshukuru Rais Dk John Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuongoza shirika hilo kongwe nchini huku akiahidi kutumia elimu na uzoefu wake ili shirika hilo liwe msaada kwa serikali katika mapambano dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi.

Pondamali aishtaki Young Africans
Bigirimana kutua Afrika Kusini