*Waziri Jafo apiga ‘stop’ ufyekaji wa msitu Uyui

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo Waziri Jafo amepiga marufuku shughuli za ufyekaji wa msitu katika Kijiji cha Kalangasi wilayani Uyui mkoani Tabora.

Dkt. Jafo amechukua hatua hiyo leo Januari 21, 2022 wakati wa ziara ya kikazi ambapo amebaini kiasi kikubwa cha miti kimeanza kukatwa kwa ajili ya mradi wa kilimo cha korosho.

Akizungumza akiwa katika eneo hilo la msitu wenye ekari takriban 4,500 alionesha kushangazwa na kitendo hicho cha kufyeka msitu na kuhoji kuwa hakuna eneo lingine la kufanya mradi huo akisema kuwa hiyo ni dhuluma kwasababu umehifadhiwa na mababu zetu ili uwe na faida kwa vizazi.

“Wazo la kuanzisha kilimo cha korosho ni zuri lakini sidhani kama hili jambo mnalotaka kulifanya ni sahihi hasa ukizngatia mimi nikiwa ni mtu niliyepewa dhamana ya kulinda mazingira na msitu huu kama mlivyoeleza katika taarifa yenu uko Manyoni na hapa, ni bora tuliache libaki kuwa eneo la hifadhi, nasema sitaruhusu msitu huu usafishwe,” alisema.

“Jana tu nilizindua Kampeni ya upandaji miti kwa wanafunzi kote nchi ili kuwafanya wawe na moyo wa kutunza mazingira sasa leo hii sisi wazazi tutaonekana wa ajabu tukianza kufyeka miti kwa hali ya juukwa lengo la kukabiliana na changamoto hizo,” aliongeza.

Aidha, waziri huyo aliuagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuangalia namna ya kuanzisha mradi mkubwa wa ufugaji wa nyuki wa kisasa ili msitu huo unufaishe wanakijiji hao.

Shehena ya parachichi yaelekea India
Waziri Ndaki atoa maelekeezo kwa wakusanya maduhuli ya serikali