Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Selemani Jafo, amewataka Watanzania kuungana pamoja na kuendelea kuliombea taifa na kumuomba Mungu, atuepushe na majanga kama yanayojitokeza kwa sasa.

Ameyasema hayo wakati wa swala ya Eid- El – Adh’aa, iliyofanyika katika viwanja vya Masjid Kibadeni Ilala jijini Dar es salaam, ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania, kuwaombea waliotangulia mbele za haki.

“Janga hili la juzi linatukumbusha janga lililotokea katika Kijiji cha Isongore Mkoani Mbeya miaka ya nyuma, lilitokea na watu wengi walipoteza maisha, janga kama hili si Tanzania pekee, sehemu nyingine kama Ghana, Nigeria, Congo limeshawahi kutokea,” amesema Waziri Jafo.

Waziri Jafo amesisitiza kuendelea kufanya maombi makubwa kwa Tanzania ili kuweza kuiokoa nchi katika majanga ambayo yanaweza kutokea.

Exclusive: Waziri Mhagama, Askofu Mkude waelezea funzo la ajali ya Morogoro (Video)
LIVE: JAMES MBATIA AKIZUNGUMZIA AJALI YA LORI MOROGORO