Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dk Selemani Jafo amezishauri halmashauri ziwatumie na ziwawezeshe vijana katika kuanzisha vitalu vya miche kwa ajili ya kupandwa maeneo mbalimbali.

Ametoa ushauri huo leo Januari 25, 2022 alipotembelea kitalu cha miche katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakati wa ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za uhifadhi wa mazingira.

Dk Jafo alishauri halmashauri hizo zipanue wigo wa bajeti zao na kuviwezesha vikundi hivyo ili viweze kuotesha miche ili kusaidia kukutatua changamoto ya uhaba wa miche.

“Mnapokuwa na vikundi vya vijana wanaootesha miche kutasaidia kuhifadhi maqzingira na wakati huo watakuwa wanapata ajira kupitia biashara ya miche ambayo wataziuzia taasisi na hata halmashauri zingine,” alisema.

Waziri wa Uingereza akumbwa na shinikizo lingine
Machinga watambulika rasmi kama kundi maalumu