Baada ya Mshambuliaji Waziri Junior Shentembo kuvunja mkataba na Young Africans, vilabu vinne vya Tanzania Bara vimeripotiwa kumuwania.

Warizi Junior aliutaka Uongozi wa Young Africans kuvunja mkataba wake, ili akatafute changamoto mpya ya kisoka nje ya klabu hiyo kongwe nchini.

Meneja wa Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Toto Africans, Azam FC na Mbao FC Juma Ismail amethibitisha uwepo wa ofa kutoka kwenye vilabu hivyo vinne, ambapo hata hivyo hakutaka kuvitaja hadharani.

“Tumepokea ofa kutoka kwenye vilabu vinne vya Tanzania Bara, tunaendelea kutafakari na siku si nyingi tutaikubali moja ya ofa hizo, “

“Ni mapema kwa sasa kuvitaja hivyo vilabu, lakini tambueni Waziri amepata ofa zaidi ya moja baada ya kuvunja mkataba wake na Young Africans.” amesema Juma.

Hatua ya kuvunja mkataba na Young Africans inamuwezesha Waziri kuwa mchezaji huru, na maamuzi ya kujiunga na klabu yoyote kwa sasa yatakuwa ni maamuzi yake binafsi.

Nichukue fursa hii kuwashukuru sana wana Yanga kuanzia makocha, wachezaji, viongozi na mashabiki kwa kuniamini na kuwa mmoja wao

Haikuwa safari rahisi licha ya kuwa fupi mno

Nilifika Yanga SC nikiwa na malengo makubwa lakini haikwenda kama nilivyotarajia labda kwa sababu zangu binafsi au vinginevyo

Ni kawaida yetu sisi wanasoka kukutana na changamoto kama hizi.

Nimechukua maumuzi mgumu sana kwangu lakini yote ni kwa maslahi mapana ya ufanisi wangu

Nimeona nihamishie jitihada zangu sehemu nyingine

Yamkini sikufikia malengo ya klabu na kutokuwapa mashabiki ile furaha waliyotarajia kutoka kwangu lakini niwatoe shaka kuwa haikuwa dhamira yangu kuwaangusha

Niwatakie kila la kheri kwenye safari yenu kuelekea msimu ujao. Tuendelee kuombeana labda ipo siku tutakuwa pamoja tena kama sio, basi nitaendelea kuuenzi upendo na imani mliyoijenga kwangu

Najivunia kuvaa nembo ya Klabu Kubwa hapa nchini. Asante (mungu kwanza) @wazir_junior_10

Tanzania Prisons yatema wachezaji 16
FAR Rabat yathibitisha kukipiga na Simba SC