Mshambuliaji wa kutumainiwa Mbao FC, Waziri Junior Shentembo amekiri katika mchezo wao wa leo dhidi ya Mabingwa Tanzania Bara Simba SC watakuwa na kibarua kigumu kuhakikisha wanatoka na ushindi, lakini wapo tayari kupambana.

Junior amesema timu yao ipo sehemu mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo njia pekee ya kuwasaidia kutoka chini ni ushindi katika mchezo unaochezwa leo jijini Dar es salaam.

“Tunajua kabisa kwamba wapinzani wetu hawataki kupoteza katika mchezo huu lakini na sisi kwetu ndio hivyo hivyo, ushindi au sare ni muhimu kwetu kuliko kupoteza,”

Junior amesema Simba hawana cha kupoteza katika mchezo huo, lakini anajua kabisa kwamba watataka kuendeleza matokeo mazuri tu.

Mshambuliaji huyo ndio kinara wa mabao katika klabu hiyo akifunga mabao kui na moja (11), huku katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Mbao FC wakifungwa mabao mawili kwa moja  na Simba, Junior alifunga bao la kufutia machozi.

Mbao FC inashika nafasi ya 19 wakiwa na alama 35 huku Simba wakiwa wanashika nafasi ya kwanza wakiwa na alama 81, wote wamecheza michezo 34.

Jurgen Klopp awabwatukia wachezaji
Fainali za kombe la dunia 2022 kuanza Novemba