Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amekutana na kupokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule wasio na makazi hapa nchini leo Januari 28,2020 Jijini Dar es Salaam.

Mabalozi waliowasilisha nakala za hati za utambulisho ni Balozi wa Ureno Mhe. Balozi Maria Amelia Maio de Paiva mwenye makazi jijini Maputo, Balozi wa Ufilipino, Mhe. Balozi Alex G. Chua ambae makazi yake yapo jijini Nairobi, Balozi wa Jamaica Mhe. Balozi Angela Veronica Comfort mwenye makazi jijini Pretoria na Balozi wa Austria, Mhe. Balozi Dkt. Christian Fellner ambae makazi yake Nairobi.

Wengine ni Balozi wa Ghana Mhe. Fransisca Ashietey-Odunton mwenye makazi Jijini Nairobi, Balozi wa Venezuele, Mhe. Jesús Agustin Manzanilla Puppo ambae makazi yake yapo Jijini Nairobi pamoja na Balozi wa Djibouti Mhe. Balozi Yacin Elmi Bouh mwenye makazi Nairobi.

Awali kabla ya kukabidhi hati za utambulisho kwa Mhe. Waziri, Mabalozi wateule walipata semina kutoka kwa Mkuu wa Itifaki, wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge.

Video: Kangi Lugola chini ya ulinzi, Hili ndilo zigo la Simbachawene
Mbwana Samatta akabidhiwa mikoba Leicester City