Ukaguzi wa Kasi ya kusambaza Umeme chini, hivi karibuni umechukua sura mpya baada ya Waziri wa Nishati kuanza kutembelea nyumba za wakazi takribani 20 zilizopo katika Kijiji Cha Usagara na Isamilo,Mkoani Mwanza zilizopo maeneo yenye umeme lakini zenyewe zikiwa hazina Umeme.

Waziri Medard Kalemani amefanya ziara hiyo juni 26 mwaka huu akiambatana na viongozi wa Tanesco Mkoa wa Mwanza, katika ukaguzi huo amebaini sababu mbalimbali ikiwemo wananchi kutokufanya “wiring” pamoja na kutokujua utaratibu wa kupata huduma ya Umeme.

“Nimegundua kuwa wananchi hawanataarifa za kutosha kuhusiana na utaratibu wa kupata huduma ya umeme, hivyo niagize TANESCO kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya taratibu za kupata umeme na kufanya uhamasishaji, haiwezekani miundombinu ifike mpaka mlangoni na bado mtu asipate Umeme”. amesema Dkt.Kaleman .

Aidha amewataka wenye nyumba kufanya “wiring” kwenye nyumba zao, na Kama nyumba zao ni ndogo watumie kifaa maalum Cha Umeme tayari (UMETA).

“Wananchi suala la kuweka umeme ni Jambo la muhimu, Serikali imebeba gharama kubwa na nyie mnachanngia kiasi tu Cha Shilingi elfu 27, lipieni muwekewe Umeme ” amesema waziri na kuitaka TANESCO kuhakikisha maeneo hayo yaliyopo pembezoni mwa Barabara yawekewe Umeme ndani ya Siku Saba tu.

Trump atupiwa lawama kampeni na ubaguzi wa rangi
Kidato cha sita waanza mitihani, shule zafunguliwa