Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Isack Kamwelwe amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli uwekwe utaratibu kwa ajili ya kulifanyia ukarabati wa Jengo la pili la abiria ili liwe na uwezo wa kubeba abiria wengi zaidi.

Ameyasema hayo leo Agosti 1 jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Jengo la tatu la abiria (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jjulius Nyerere. (JNIA)

‘Ombi langu kwako Rais, jengo lile Terminali II linahitaji mambo mawili, moja kulikarabati lipendeze kama ambavyo wamependeza wananchi waliokusanyika hapa, kama alivyosema Makonda ‘Wameoga’ lifanyiwe marekebisho ili nalenyewe ling’are kama jengo la tatu lilivyo, pili katika kukarabati huko liongezewa uwezo ikiwezekana mara mbili badala ya kubeba abiria milioni 1.5 libebe abiria milioni 3” amesema Waziri Kamwelwe.

Hata hivyo, Jengo la tatu la abiria (TERMINAL III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 560 na litakuwa na uwezo wa kubeba abiria milioni 6 kwa mwaka.

 

 

Magufuli amtengua DED Halmashauri ya Wilaya Morogoro
Mtoto wa Osama, Hamza Bin Laden Ameuawa