Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji amemtaka Mtanzania Mbunifu Masoud Kipanya kuandika barua SIDO ili waweze kuwaandikia TBS na kuweza kutoa Cheti cha Ubora wa gari ambalo amelibuni hivi karibuni.

Waziri Kijaji amesema hayo mara baada ya ziara yake katika Shirika la Viwango Tanzania na kujionea gari ambalo amelibuni Masoud Kipanya likifanyiwa tathimini ya ubora wa viwango.

Amesema kuna mambo madogo yanahitaji kurekebishwa kwenye gari hilo hivyo Masoud Kipanya atakaa na wahandisi wa TBS ili waweze kuelekezana ili gari liweze kupita katika barabara zote kwani jinsi ilivyo inaweza ikapita na ikaumia kwa muda mfupi.

“Tunataka kukaa nae ili aweze kutengeneza chombo ambacho sasa kitaweza kutumika kwenye uhitaji wa soko letu lilivyo na sisi kama wizara tunasimamia kuona anafikia kwenye viwango vizuri na kwa mara ya kwanza tuseme tuna gari letu ndani ya taifa letu”. Amesema Waziri Kijaji.

Aidha Waziri Kijaji amesema serikali inawatambua wabunifu wote ambao wapo katika jamii na wizara imejipanga kuanza kuwafikia vijana wabunifu wakitanzania kuanzia kwenye fikra zao mpaka kufikia kuwajenga hatua kwa hatua.

Mkurugenzi wa Upimaji na Ugezi TBS Mhandisi Johanes Maganga amesema wanaendelea kutekeleza majukumu yao  na mpaka sasa matokeo ya awamu ya kwanza yameshatoka na maelekezo ambayo wamepatiwa na Waziri wanaenda kuafanyia kazi kuanzia sasa.

“TBS kwa kushirikiana na Masoud Kipanya tutakaa nae tutaangalia ninamna gani ambavyo anaweza akafanya malekebisho hayo kwa muda mfupi kwamaana hatutaki achelewe  alafu aanze uzalishaji wa magari  mengine ambayo ameshaanza kuyatengeneza”. Amesema 

Sakho: Muda wa kulipa kisasi umewadia
Kocha Pablo kuendelea Simba SC