Katika kuhakikisha kuwa Serikali ya awamu ya tano imejipanga kushughulikia na kumaliza tatizo la ardhi nchini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amejikuta akikesha mara baada ya wananchi takribani 189 kumwuomba asitoke ofosini kwake ili aweze kuwasaidi kuondokana na kero ya ardhi ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu.

Waziri huyo wa ardhi  ametumia takriban saa 20 kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake hadi kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi ndipo alipojikuta akikesha na wananchi ofisini kwake.

Aidha, Wananachi wengi wenye matatizo na Kero za ardhi kutoka maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar es salaam kwa ujumla wametumia fursa hiyo ya kipekee ya kuonana na Waziri mwenye dhamana ya Ardhi na kumuelezea kero zao na hatimaye kupatiwa ufumbuzi papo hapo.

Hata hivyo, Mwanzoni mwa mwezi Juni 2017, Lukuvi alitoa Tangazo la kuwataka wakazi wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani ambao wangependa kuonana nae wafike katika ofisi yake ya kanda ya Dar es Salaam iliyopo Wizara ya Ardhi – Magogoni ili kujiandikisha majina yao, anuani na namba zao za simu.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari awasili Zanzibar kuhudhuria Tamasha la ZIFF
Serikali yaipongeza Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni PPF