Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  January Makamba ameitaka jamii ya watu wa Parakuyo waliopo Wilaya ya Kilosa kuishi kwa amani, uvumilivu na upendo miongoni mwao kwani ndio misingi ya watanzania.

Ameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara uliojumuisha jamii za wakulima na wafugaji ambazo zimekuwa na migogoro ya mara kwa mara na kuzitaka jamii hizo kuishi kwa amani na kuhifadhi mazingira kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Makamba ameuagiza uongozi wa Wilaya na Kijiji kushirikiana pamoja kuunda kamati ya Amani itakayokuwa na wajumbe kutoka pande zote mbili za wakulima na wafugaji na viongozi wa madhehebu ya dini ili kutafuta suluhu ya kudumu baina ya pande mbili ambazo zimekua na migogoro ya mara kwa mara. “Undeni Kamati hii mapema na Ofisi yangu itagharamia mafunzo kwa Kamati husika juu ya namna bora ya kutatua migogoro” Alisema Waziri Makamba.

katika jitihada za kukuza uelewa wa masuala ya mazingira na changamoto zake,  Makamba ameitaka Serikali ya Kijiji kuunda Kamati ndogondogo za Mazingira ambazo zipo kwa mujibu wa sheria ya Mazingira na kuahidi kuipati mafunzo Kamati hizo ikiwa ni pamoja na kutengeneza sheria ndogo ndogo zitakazotumika kama nyenzo ya kuhifadhi na kusimamia Mazingira ya maeneo yao.

Aidha,  amesema kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ni muhimu sana na kuitaka jamii ya Parakuyo na Twa twa twa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuhakiki na kuhesabu mifugo yako ili kubaini ni ardhi kiasi gani inahitajika kwa wakulima na kiasi gani kwa wafugaji. “ndugu zangu niwasihi, Serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha kuna kuwa na matumizi bora ya ardhi, hivyo nawashauri mmshiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupata uwiano wa idadi ya mifugo na ardhi iliyopo”alisisistiza Makamba .

Awali katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Morogoro  Makamba pia alitembelea chanzo cha maji na kujionea changamoto za kimazingira katika mto Mambogo.

Jose Mourinho Afunguka Kuhusu Mwamuzi Anthon Taylor
Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo afanya ziara ya Kushtukiza