Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba jana amefika makao makuu ya jeshi la polisi kuandikisha maelezo kuhusiana na sakata la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji.

Akithibitisha kuhojiwa kwa Makamba, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa alifika kituoni hapo ili kuchukuliwa maelezo kuhusu suala la mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ aliyetekwa Oktoba 11 na kupatikana Oktoba 20, 2018.

“Alifika jana kwaajili ya kuchukuliwa maelezo kuhusiana na suala la kutekwa kwa mfanyabishara Mo Dewji, kuna mambo tulitaka kuyapata kutoka kwake kwaajili ya taarifa,”amesema Mambosasa.

Aidha, mfanyabishara, Mohammed Dewji alitekwa na watu wasiojulikana Alfajiri ya Oktoba 11, wakati akiwa mazoezini Collesium hotel na baadae Oktoba 20 alipatikana akiwa ametelekezwa katika viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam.

Lema ajisalimisha kituo cha polisi
Prof. Ndalichako aagiza waliofutiwa usajili UDSM warejeshwe

Comments

comments