Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian leo kwa mara ya kwanza amekiri kuwa nchi yake iliipa Urusi ndege zisizo na rubani, akisisitiza kuwa hatua hiyo ilifanyika kabla ya vita vya Ukraine na Urusi eneo ambalo ndege hizo zimeshuhudiwa zikitumika.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Theran, Waziri Hossein amesema walitoa idadi ndogo ya ndege hizo ikiwa miezi kadhaa kabla ya vita hivyo kuanza.

Ndege isiyo na Rubani maarufu kama Kamikaze. Picha ya Reuters

Kauli ya waziri huyo inatolewa baada ya miezi kadhaa ya taarifa zenye utata kutoka Iran kuhusu usafirishaji wa silaha hizo, huku Urusi ikizitumia ndege zisizo na rubani kushambulia vituo vya nishati vya Ukraine, miundombinu na makazi ya raia.

Awali kulikuwa na tetesi kuwa taifa hilo linaisaidia urusi kwa kuipatia ndege zisizo na rubani ambazo zimekuwa zikifanya mashambulizi nchini Ukraine na kusababisha uharibifu wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ile ya umeme.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 6, 2022  
Zelensky ajipa matumaini vita yake na Urusi