Taasisi ya Kupambana na Rushwa, Lesotho inawafanyia uchunguzi Waziri Mkuu, Thomas Thabane na mwanae, Potlako, kwa tuhuma za rushwa kubwa na utakatishaji wa fedha.

Taarifa hizo zimetolewa na  Serikali ya Lesotho ikieleza kuwa uchunguzi huo unaendelea kufanyika kwa tahadhali kali.

Waziri mkuu huyo na mwanae wamekuwa wakituhumiwa kuhusika kuhujumu uchumi wa Lesotho, ingawa ofisi yake imekuwa akikanusha kuhusika na tuhuma hizo za rushwa.

Msemaji wa taasisi ya kupambana na rushwa, Matlhokomelo Senoko amesema uchunguzi huo unafanywa kwa ustadi na staha kwa kuwa bado ni tuhuma na kwamba unafanyika kwa lengo la kupata ukweli na siyo kuharibu jina na hadhi ya mhusika.

Kiongozi huyo na kijana wake wamekuwa wakituhumiwa kupokea pesa za rushwa kutoka familia ya wafanyabiashara wakubwa wa Afrika Kusini, maarufu kwa jina la The Gupta’s.

Wanatuhumiwa kuuza kwa ‘bei chee’ baadhi ya migodi ya madini na ardhi kubwa kwa The Gupta’s.

 

Majaliwa: Ukikutwa na mwanafunzi wa kike nyumbani kwako jela miaka 30
Polepole amjibu Mbowe, ‘watoto wake wako wapi’