Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Temeke kuondoa wafanyakazi wa mkataba kwa njia ya kuwapa ajira ya kudumu kwa wenye sifa na kuwa ondoa wasio kuwa na sifa ifikapo  Julai 30 mwaka huu.

Amesema kitendo cha kuto waajiri na kuwatumikisha kwa mikataba kwa muda mrefu kinasababisha wakose stahiki zao jambo ambalo si halikubaliki.

Aidha waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo  wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na ku sisitiza kwamba ni lazima suala hilo lishughulikiwe haraka kwa sababu hayo ndio matundu ya watumishi hewa.

“Mnawatumikisha watu kama vibarua kwa muda mrefu, hapa kuna wengine wanafanya kazi kwa mikataba kwa miaka mitano hadi sita hii haikubaliki kwani mnawakosesha stahili zao pale mnapo waachisha kazi,” alisema.

Awali Kaimu Afisa Utumishi wa Manispaa hiyo Zaitun Hassan alisema kuwa wamekuwa wakitoa ajira za mikataba kwa sababu wamekosa watu wenye sifa za kuweza kuajiriwa hususani madereva.                                                          Zaitun aliongeza kuwa madereva wengi wanaojitokeza pindi wanapotangaza ajira wana shindwa kufikia vigezo ikiwemo kuwa na cheti cha VETA na badala yake wanakuwa na cheti cha kidato cha nne tu.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa kuna wafanyakazi wengine katika Idara ya Uhasibu na Ujenzi ambao nao wameajiriwa kwa mkataba hivyo amemtaka Afisa Utumishi kuomba kibali cha kuajiri kwa Katibu Mkuu Utumishi.

Mh.Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kufanya tathmini ya maeneo yote ya shule kwenye mkoa wake na watakaobainika kuingia katika maeneo hayo waondolewe haraka.

Waziri mkuu aliongeza kuwa baada ya kukamilisha utengenezaji wa madawati kinacho fuatia sasa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambapo amezitaka halmashauri kuweka mipango  ya kujenga majengo ya madarasa ya ghorofa ili waweze kuwa na madarasa mengi katika eneo dogo.

Awali Mh.Majaliwa alipokea msaada wa madawati 705 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Chamazi wilaya ya Temeke ambapo kati yake Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania umetoa madawati 600 na Jumuiya ya Mabohora imetoa madawati 105.

Pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Agustino Mahiga alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 85 fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati.

Dk. Mahiga alisema watumishi hao walichanga sh. milioni 100 kwa ajili ya utengenezaji wa madawati ambapo sh. milioni 15 wamekabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe ambaye alikuwa mtumishi wa wizara hiyo ili kutatua tatizo la madawati kwa shule za wilayani kwake.

Kwa upande wake Balozi wa Kuwait nchini Jaseem Al Najem amesema Serikali ya Kuwait itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika shughuli zote za maendeleo hususani katika sekta za elimu na afya.

Jaji Mutungi Akemea Tamko La Chadema
Mrisho Mpoto akunwa na nyimbo za Nay wa Mitego 'aliyefungiwa', amshauri