Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amesema kuwa baadhi wa wanajeshi walioandamana hadi ofisini kwake wiki iliyopita walipanga kumuua.

Kiongozi huyo ameliambia Bunge la nchi hiyo kuwa aliamua kuwatuliza kwa kuwataka wapige push-up kwanza na yeye akajiunga nao, lakini hawakuwa na nia njema.

Ingawa Waziri Mkuu huyo alionekana akicheka na wanajeshi hao alipokuwa anapiga push-up, ameliambia Bunge kuwa alikuwa anacheka nje lakini ndani yake hakuwa na furaha.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed

Miezi sita iliyopita, alifanya mabadiliko ambayo amedai kuwa baadhi ya vikosi vya jeshi havikuyapenda na vilitaka kugoma.

“Maandamano ya wanajeshi kwenye ofisi yangu ambayo ni Ikulu ya nchi, sio tu kwamba kilikuwa kinyume cha sheria lakini pia kilikuwa kitendo cha hatari sana, kwa sababu lengo lao lilikuwa kugomea mabadiliko niliyoyaleta,” Waziri Mkuu Abiy aliliambia Bunge.

“Baada ya kudhibiti hali pale ofisini kwangu, baadhi ya wanajeshi walisikika wakisema, ‘ana bahati ametoroka kabla hatujamuua’,” aliongeza.

Alisema kuwa kitendo kile kilimfanya afikirie kuwa huenda kukatokea machafuko kwani vijana wanajeshi walikuwa wakiandamana kwenda Addis Ababa. Hali iliyokumbushia harufu ya vita vya kikablia nchini humo.

Wengi wameonesha kushangazwa na tamko la Waziri Mkuu ambalo ni tofauti na alivyosema wiki iliyopita wakati wa tukio hilo.

Mwana FA, Richie wateuliwa kuwa wajumbe Bodi ya BASATA
Azam FC yaanza kuipigia hesabu Singida United

Comments

comments