Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano, Kassim Majaliwa leo Febuari 6, 2020 bungeni jijini Dodoma amesema kuwa hakuna chama chochote cha siasa kilichozuiliwa kufanya shughuli zake za kisiasa ila tu umewekwa utaratibu maalumu kwa ajili ya kuendesha shughuli za kisiasa na utaratibu huo unatakiwa kufuatwa na vyama vyote vya siasa hapa nchini.

”Vyama vya siasa havijazuiwa kufanya shughuli zake, ila tumeweka taratibu muhimu unaowezesha vyama kufanya shughuli zake za kisiasa kama ambavyo tumetoa, kumekuwa na uhuru pia wa wale wote wanasiasa waliomba ridhaa kwenye maeneo yao wakapata ridhaa hiyo kuendelea kufanya shughuli kwenye maeneo yao kama ambavyo wao wanapaswa kufanya shughuli hizo.

Ametoa majibu hayo kufutia swali la mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe kuhoji mbele ya Bunge takatifu kuwa ni lini serikali itaruhusu vyama vya siasa kufanya shughuli zao za vyama hasa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, ikiwa zimebaki siku 262 tu.

”Ni miaka minne sasa tangu Serikali imeweka zuio kwa vyama vya siasa kufanya wajibu wake kw amujibu wa katiba na sheria za n chi, na tunapozungumz aleo mkuu zimebaki siku 262 zimebaki kufika taehe 25 oktoba nchi yetu kufanya uchaguzi i wa rais, wabunge na madiwani, Mheshiwiw wairo mkuu kwa busara zako binfasi na za serikali amabyo wewe ni kiongozi mwandamizi mnafikiri ni lini mtaruhusu vyam avya siasa vifany wajibu wake wa uenezi kujianda na uchaguzi mkuu” amehoji Mbowe.

Ambapo Waziri akitolea ufafanuzi wa kina ameongezea kuwa ratiba za kufanya uchaguzi na kampeni zitatolewa kama ilivyokawaida hivyo vyama viendelee kufuata kanuni na taratibu za nchi kama zinavyoelekeza.

”Ratiba za uchaguzi zitatotelwa na ratiba hizo zitaeleza kuanzia lini shughuli za kampeni zitaanza mpaka lini ili chama zikaeleze sera zake kwenye maeneo yote ili sasa wananchi waweze kupata fursa kuendelea kufanya uamuzi wa sera ipi ya chama gani inaweza kutuletea maendeleo ya nchi” amezungumza Waziri Kassim Majaliwa.

Aidha swali hilo limejili kufuata mfululizo wa matukio ya vyama vya upinzani kuandaa mikutano ya kisiasa inayokuja kuzuiliwa na jeshi la polisi na kupewa barua za kuzuia kufanyika kwa mikutano hiyo, hivyo Mbowe ameamua aulize ili aweze kupata majibu ya moja kwa moja kufuatia kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi wa Rais, wabunge pamoja na madiwani.

Vigogo kukutana robo fainali ligi ya mabingwa, kombe la shirikisho Afrika
Eric Abidal anusuru kibarua chake FC Barcelona