Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amewasisitiza Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona, ambapo amewataka kuzingatia kwa kufuata taratibu za Wizara ya afya na kufanya yale yanayoweza kupunguza maambukizi ikiwemo kujifukiza, kutumia juisi ya tangawizi, maliamao pamoja na kufanya mazoezi.

Amesema hayo leo leo Julai 21, 2021 wakati wa ibada ya Sikukuu ya Eid Al Adha iliyofanyika katika Msikiti wa Mtoro jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kuwa ugonjwa upo nchini hivyo ni lazima watanzania wajue umuhuimu wa kujikinga pamoja na kuomba Mungu.

“Tunao wagonjwa wachache tuendelee kuwaombea jukumu la Serikali ni kutoa huduma kwa wanaofikwa na ugonjwa huu, lakini pia tusiache kujikinga,”amesema Majaliwa

“Tuchukue tahadhari kwa kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono, pamoja na kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko. Pia tuendelee kujikinga kwa kufanya mazoezi, juisi yetu ile tusiiache, lakini pia kukaa kwenye joto ambapo tuliipa jina la nyungu nayo itumike ili kupambana na ugonjwa huu,” amesema Majaliwa

Aidha amesema kuwa kuhusu Chanjo ipo na kwamba anayetaka akachanje kwani hakuna atakayelazimishwa kupata chanjo ni hiari.

“Tumesema kuchanja ni hiari, hivyo kama unataka kuchanja nenda mahali zilipo. Kama unaona umuhimu mwakani kwenda Hijja, una watoto wanasoma nje ya nchi na hairuhusiwi kwenda mpaka uwe umechanjwa basi fursa ipo hapa hapa usiangaike kwenda nje,” amesema Majaliwa

COSOTA watakiwa kutoa elimu ngazi za mikoa
Naibu Waziri amuonya mkandarasi ''Hatutaongeza muda''