Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro na naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji, William Tate Ole Nasha yaliyofanyika leo nyumbani kwa Marehemu Kijiji cha Osinoni kata ya Kakesyo wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

Majaliwa ambae amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu akiongozana na Spika wa Bunge Job Ndugai, amewasihi wananchi wamuenzi kwa kuyaendeleza mambo mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake na kuongeza kuwa kifo cha Ole Nasha ni pigo kwa Serikali na Chama cha Mapinduzi.

Aidha Waziri Mkuu amesema Rais Samia anawataka watanzania waenzi mambo mazuri yote aliyoyaacha yanayonufaisha jamii yake na michango mingi aliyoifanya ya hali ya juu kwa Serikali.

Amesema Jambo la Muhimu kwa sasa ni kuendelea kumuombea Marehemu na kumuomba mwenyezi Mungu amlaze mahali pema.

“Mke wa Marehemu, watoto, ndugu, jamaa, na wabunge nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape Moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu”.

William Tate Ole Nasha alifariki ghafla siku ya Jumatatu septemba 27, 2021 mkoani Dodoma akiwa nyumbani kwake.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 3, 2021
Classic Finishes Suluhu gharama za vigae