Waziri Mkuu wa Finland, Sanna Marin (36), ​​amekumbwa na kashfa baada ya video zake akicheza bila hiyana kwa mtindo wa kukata nyonga kwenye karamu kuvuja mwezi huu, na kusababisha mzozo wa kimtazamo ambapo wengi wa wananchi na baadhi ya Viongozi wanamtaka ajiuzuru.

Baadhi ya Wafini, wamekuwa wakipigia kelele za kutaka Marin ajiuzulu kutokana na tukio hilo, wakisema kwamba mwenendo wake haufai kwa cheo alichonacho cha Uwaziri Mkuu, huku wengine wakimuona kama ni mhamasishaji wa siasa za kisasa kulingana na umri wake.

Suala hilo, pia limeibua swali la iwapo Marin anashauriwa vyema na viongozi wazee wa kiume waliowahi kushika nyadhifa Serikalini, huku aliyekuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Finland, Tarja Halonen akisema, “Hii inaumiza aina fulani ya mwanaume mzee.”

Inadaiwa kuwa, hata kwa viwango vya Kifini Marin bado ni mchanga kiumri na serikali yake ni ya kike kipekee na kwamba alipoingia madarakani mwaka wa 2019, akiwa na umri wa miaka 34, alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 20 kuliko watangulizi wake wawili wa kiume.

Marin, ameongoza Ufini kupitia adha ya janga la Uviko-19 kuwa ni moja ya nchi yenye viwango vya chini vya vifo barani Uropa, baada ya Urusi kuivamia Ukraine na alisafiri hadi Uswidi ili kupata uungwaji mkono kwa jitihada kubwa za Ufini na Uswidi za kujiunga na NATO.

Hata hivyo, Sanna Marin amejitokeza katika vyombo vya Habari na kudai kuwa anatazamia kupata vipimo vya Dawa za kulevya iwapo alitumia katika vinywaji au vyakula alivyotumia wakati wa tafrija aliyohudhuria na kupelekea kufanya tukio hilo.

PSPTB:Wanunuzi wa Umma wasiojisajili watasaga meno
Serengeti Girls kuweka kambi England