Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ameziagiza taasisi za Serikali ambazo hazijaanza kutoa huduma kupitia vituo vya huduma Pamoja vya shirika la posta Tanzania zihakikishe zinaanza kutoa huduma katika vituo hivyo ndani ya mwaka huu wa fedha.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Septemba 6, 2021 wakati akizindua vituo vya huduma pamoja vya shirika la posta Tanzania kwenye viwanja vya posta makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Aidha Majaliwa ameitaka Wizara ya Fedha kupitia madeni ya wadaiwa wote ili kuhakikisha wanalipa madeni yao jambo ambalo litaimarisha shirika hilo.

Amesema baadhi ya taasisi hizo ni tume ya ajira, kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), Shirika la viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Huduma pamoja ni vituo vitakavyotoa huduma zote za Serikali katika eneo moja kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma mbalimbali na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Taasisi ambazo tayari zimeanza kutoa huduma kupitia vituo hivyo ni RITA, UHAMIAJI, NIDA, BRELA, TRA, PSSSF, NSSF na Halmashauri za Majiji, Waziri ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupata huduma ambapo kwa sasa huduma hizo zinatolewa katika vituo vilivyopo kwenye Oofisi za Posta  jijini Dara es Salaam na Dodoma.

Maadhimisho siku ya wazee
Waziri Gwajima azindua kliniki tembezi za magonjwa ya TB