Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam mapema leo na kubaini upotevu wa makontena 349.

Duru zimeeleza kuwa Waziri Mkuu alibaini upotevu wa makontena hayo ambayo yana thamani ya zaidi ya shilling bilioni 80, na kuagiza kufutwa kazi mara moja kwa maafisa waliohusika na upotevu huo.

Aidha, taarifa zimeeleza kuwa Majaliwa amewasimamisha kazi Kamishna wa Kodi, Tiagi Masamaki pamona na Habibu Mpozya wa kitengo cha huduma kwa wateja.

Uamuzi huo wa Waziri Mkuu ulikuja baada ya kubaini kuwa katika kumbukumbu za Mamlaka ya Bandari kuna taarifa ya makontena 349 yenye thamani ya shilingi bilioni 80 lakini taarifa hizo hazipo kwenye kumbukumbu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Waziri Mkuu alielekeza Polisi kuwakamata maafisa wote waliohusika na sakata hilo kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Milionea Aliyemuua Mtu Aliyempiga Picha Mwanae Wa Kike Asamehewa Kwenda Jela
Diamond: Sitaki kabisa kushika simu ya Zari, namjua...!