Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumatatu Julai 12, 2021 amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi.

Akiwasili katika uwanja wa Mohammed V jijini Casablanca Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokelewa na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha mahusiano hususani ya kiuchumi kati ya Tanzania na Morocco.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor, Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda na Mkurgenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Japhet Justine.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 13, 2021
RC Makala aruhusu biashara soko dogo la Kariakoo