Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwasili mjini Dodoma kesho Septemba 30,2016 mchana.

Majaliwa anawasili Dodoma kutimiza ahadi yake aliyoitoa Julai 25 2016 wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa Kitaifa Mkoani Dodoma ambapo aliahidi kuhakikisha ifikapo Septemba 2016 anahamia Dodoma kama mwanzo wa kutekeleza uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma.

Waziri Majaliwa pia atafanya ziara ya siku mbili Manispaa ya Dodoma kuanzia Oktoba mosi hadi pili 2016 kukagua hatua mbali mbali za maandalizi ya kupokea Serikali kuhamia Dodoma.

Twaweza: Asilimia 60 wanaunga mkono zuio la mikutano ya vyama vya siasa
Video: Tumejipanga vizuri kuelekea kilele cha kampeni ya Mti wangu